Wednesday, August 1, 2012

ZITTO AWAPATANISHA WASANII WA JUMBA LA DHAHABU


Zitto Kabwe.
Na Gladness Mallya
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini kwa ‘leseni’ ya Chadema, Zitto Kabwe hivi karibuni aliwapatanisha wasanii wa mchezo wa Jumba la Dhahabu na mkurugenzi wao, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ kufuatia tofauti zilizotokea nyuma.
Tukio hilo lilifanyika ndani ya Ukumbi wa THT, Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni baada ya wasanii hao kuacha kufanya kazi na Kampuni ya Chuz Entertainment.
“Namshukuru Mhe. Zitto kwa kusaidia kumaliza tofauti zetu, sasa wasanii wote tumerudi na tunafanya mazoezi kwa ajili ya kucheza Jumba la Dhahabu Season II,” alisema Chuz.
Gazeti hili lilishuhudia wasanii mbalimbali wa zamani wakiendelea na mazoezi maeneo ya Mwananyamala ilipo ofisi ya kampuni hiyo. Wasanii hao ni Angel John Komba ‘Winter’, Cecilia Sengerema ‘Mamtei’, Bajomba na wengine kibao.

No comments:

Post a Comment