Wednesday, August 29, 2012

TAARIFA KAMILI KUHUSU DIDIER DROGBA KUONEKANA TENA CHELSEA.


2
.
Mtandao wa Give me football umeripoti kwamba Mkali wa soka Didier Drogba ambae baada ya mkataba wake na Chelsea kuisha alisain dili jipya na club ya Shenhua ya China, amerudi na kuonekana kwenye mazoezi na Chelsea.
Katika kipindi hiki cha mapumziko kwenye msimu wa soka China, Drogba amerudi London kuisalimia familia yake lakini pia alionekana kwenye uwanja wa mazoezi na Chelsea.
Give me Football wamezidi kutiririka kwamba kuna uwezekano huo ndio ukawa mwisho wa Drogba kuichezea Shenhua baada ya kugundulika kwamba club hiyo inahangaika kutafuta pesa za kuendelea kuwalipa wachezaji wake kutokana na pesa nyingi kutolewa kwa mishahara ya Drogba na Anelka.
Kutokana na club hiyo kuwa na tatizo la kifedha kwa sasa upo uwezekano mkubwa wa Drogba na Anelka kuuzwa kwenye club nyingine ili angalau hizo pesa zisaidie kuiokoa Shenhua, kutokana na hilo pia kwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa Drogba kurudi kuichezea Chelsea kama itakubali kuilipa Shenhua.

No comments:

Post a Comment