Friday, August 3, 2012

SKENDO YA RUSHWA KWA WABUNGE, HAPONI MTU


Christopher Ole Sendeka.

Lucy Mayenga.
Athuman Mfutakamba.
Vicky Kamata.
Na Mwandishi Wetu
HALI bado tete ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea mjini Dodoma kufuatia madai ya kuwepo kwa wabunge waliokula mlungula ili kuitetea ajira ya Bosi Mkuu wa Shirika la Ugavi Tanzania (Tanesco), William Mhando ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa madai ya matumizi mabaya ya madaraka, Ijumaa limechimba.
Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa baadhi ya wabunge na viongozi wa vyama vya siasa wanapiga ‘ndogondogo’ ili waheshimiwa wanaotuhumiwa kupokea ‘kitu kidogo’ wabatilishiwe ubunge wao na serikali iitishe chaguzi ndogo ili kuziba nafasi zao.
“Unajua tatizo kubwa ni kwamba wapo baadhi ya wabunge wanaojiona wasafi na wapo viongozi wa siasa wanataka wabunge wenye kashfa watimuliwe na kwenye majimbo yao kuitishwe chaguzi ndogo.
“Hawa viongozi wa siasa (baadhi) ni wale ambao wabunge wao waliotuhumiwa ni tishio kwa maslahi yao ndiyo maana wanataka wang’oke, lakini uchunguzi umeanza, sijui kama kuna atakayepona,” alisema mbunge mmoja wa kutoka mkoa wa Arusha.
Awali majina ya wabunge hao yalikuwa siri, lakini juzikati, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu (Chadema-Singida Mashariki) aliwafungukia waheshimiwa hao kwa majina.
Lissu aliwataja Christopher ole Sendeka, Sarah Msafiri, Yusuf Nassir, Charles Mwaijage, Mariam Kisangi, Vicky Kamata na Munde Tambwe ambao wote walikuwa kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjiliwa mbali na Spika wa Bunge, Mh. Anna Semamba Makinda.
Hata hivyo, kamati hiyo pia ilikuwa ikiundwa na Selemani Zedi (Mwenyekiti), Diana Chilolo (Makamu Mw/kiti), Haji Khamis, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Dr. Festus Limbu, Athuman Mfutakamba na Lucy Mayenga.
Wengine ni Josephine Changula, Mwanamrisho Taratibu, Suleiman Nchambi, Ally Mbarouk Salim, Kisyeri Chambiri na John Mnyika.
Tayari Kamati ya Maadili, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge imeanza kufanya uchunguzi kama madai hayo yana ukweli wowote. Ikithibitika, ina maana hakuna atakayepona.

No comments:

Post a Comment