Mrisho Ngassa.
Kiungo wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na
uongozi wa timu yake. Mchezaji huyo aliyekuwa anasadikiwa kutua Yanga
SC amepelekwa Simba baada ya pande mbili za Azam FC na Simba SC kufikia
makubaliano. Wakati hatua hiyo inachukuliwa, Ngassa mwenyewe anadai hana
taarifa yoyote kutoka kwa uongozi wa timu yake ya Azam na wala
hajafanya mazungumzo yoyote na Simba. Ngassa amesema kama Azam
hawamuitaji ni bora wangekaa naye na kufuata taratibu za kuvunja mkataba
kuliko kumpeleka kama mzigo. Mchezaji huyu alikuwa na mkataba na timu
hiyo mpaka mwakani.
No comments:
Post a Comment