STAA wa filamu na muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anadaiwa kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kupenda uhusiano wa kimalavidavi na vijana wadogo a.k.a Serengeti boys anaowazidi umri.
Hot 2 Hot imenong’onezwa kuwa mwanadashosti huyo alikuwa akifanya siri lakini sasa imevuja kwamba amekuwa akibanjuka na damu changa mfano ukitolewa kwa wasanii wenye ‘eji’ ndogo ambao aliwahi kujilainisha kwao kwa kuwahonga visenti na kuwapa gari lake watembelee ‘tauni’.
Baada ya kuzitia ‘nyiuzi’ hizo masikioni, Hot 2 Hot ilimnyatia bosi huyo wa Shilole Classic na kumsomea mambo yake yote, ndipo akatanua kinywa:
“Ninavyojua mapenzi hayachagui umri mkubwa wala mdogo, nawashangaa hao wanaosema hivyo, sasa wanataka niwe na wazee? Mimi ni kijana, lazima niwe na uhusiano na vijana wenzangu.”
Imeandaliwa na Gladness Mallya, staa mwenye picha kali atupigie 0754 332033
No comments:
Post a Comment