Sunday, August 5, 2012

SIMBA YA NASA KIFAA CHA MAANA



Wilbert Molandi na Issa Mnally
KLABU ya Simba ipo katika hatua za mwisho za kumleta straika, Sihaone Abdulaziz, anayeichezea Stella Abidjan ya Ivory Coast.
Straika huyo anatarajiwa kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Rage, alisema mshambuliaji huyo ataichezea Simba msimu mmoja kabla ya kwenda nchini Hispania kucheza soka la kulipwa.
Rage alisema ataichezea klabu hiyo kwa muda kutokana na mipango yake ya kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
“Ndani ya masaa 48 tutamtambulisha mshambuliaji mpya atakayesaidiana na Felix Sunzu, ambaye ni Sihaone Abdulaziz kutoka Ivory Coast.
“Mshambuliaji huyo atatuchezea kwa muda kati ya mwaka mmoja au miwili, kutokana na mipango yake ya kwenda kucheza soka nchini Hispania,” alisema Rag

No comments:

Post a Comment