Wema na Snura.
Na Gladness MallyaUSHOSTITO wa Wema Sepetu na Snura Mushi uliodumu kwa miezi kadhaa umeraruliwa ukidaiwa kuvunjika kwa kuwa ulikuwa wa kinafiki kutokana na kuvunja kiapo walichokula runingani kuwa hatawaachana, Ijumaa Wikienda limejazwa werawera na wabaya wao.
MTU WA KARIBU ATIRIRIKA
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema na Snura walikuwa marafiki vinyonga kwani kila mtu alijua muda siyo mrefu watasalitiana na kuanza kuvujisha siri zao na hicho ndicho kilichotokea.
KISA NI NINI?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Wema alidai kuwa Snura amemsema vibaya kwa ndugu zake na kutangaza kwa wanahabari kuwa amerudiana na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, jambo ambalo lilimchukiza.
Chanzo kilitiririka kuwa baada ya urafiki huo kuvunjika, Wema alimnyang’anya Snura vitu vyote ambavyo alikuwa amemnunulia na kuanzia hapo mawasiliano baina yao yalikatika.
“Snura ameamua kuvunja kile kiapo alichokula runingani kwa machozi, sasa sijui atapata wapi yale mawigi aliyokuwa akipewa na Wema?,” kilihoji chanzo na kuingia mitini.
SNURA ANASEMAJE?
Alifunguka: “Mimi sijui sababu ya urafiki wetu kuvunjika kwa sababu Wema hajaniambia, angekuwa ni mtu mwenye akili na busara angenieleza.”
NYUMBANI KWA WEMA
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Wema lakini haikupokelewa hivyo likatimba nyumbani kwake ambapo wakiongozwa na Vincent Kigosi ‘Ray’, wasanii hao walitumia nafasi yao kumkashifu mwandishi wetu kwa maneno mabaya yasiyoandikika gazetini, tunayafanyia kazi.
No comments:
Post a Comment