Sunday, August 12, 2012

Okwi: Sijasaini Simba, naondoka


Emmanuel Okwi.
Na Wilbert Molandi
SIKU chache baada ya kujiunga na klabu yake ya Simba akitokea kwenye majaribio nchini Austria, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, amesema bado hajaongeza mkataba wa timu hiyo na pia anatarajiwa kuondoka tena kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Okwi alikuwa kwenye kikosi cha FC Red Bull ambapo alishindwa kutokana na kile alichodai kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Mchezaji huyo ameliambia gazeti hili kuwa anatarajia kurejea nchini humo kuendelea na majaribio wakati wa kipindi cha majira ya baridi.
“Nilifanya majaribio kwa siku tatu tu, kabla ya kupata malaria na muda wa usajili ulikuwa unafikia tamati huko Austria.
“Nikiwa huko nilifanya mazoezi ya pamoja na timu kwa siku hizo, baada ya hapo nikaugua lakini nitarudi, kuhusu mkataba na Simba, umesalia mwaka mmoja na bado sijasaini wa kuongeza kwa kuwa bado nipo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu yangu,” alisema Okwi.

No comments:

Post a Comment