Kelvin Yondani.
Wilbert Molandi na Issa MnallyKLABU ya Simba imeapa kuwa beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, hataichezea Jangwani katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage, katika mkutano wake mkuu uliofanyika kwenye Ukumbi wa Polisi Officer’s Mess, Masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rage alisema ana ushahidi wa mkanda wa video unaomuonyesha beki huyo akitamka kuwa yeye ni mchezaji halali wa Simba wakati akisaini mkataba.
Rage amewapa wapinzani wake wa Jangwani siku sita kuanzia jana Jumapili hadi Ijumaa kutoa Shilingi Milioni 60 za kukatisha mkataba wa beki huyo kabla ya kulifikisha suala hilo kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
“Nawaomba Yanga tukae pamoja kwa ajili ya kulimaliza suala la Yondani, tunachotaka sisi ni Shilingi Milioni 60 za uhamisho wake kwenda Jangwani vinginevyo hataichezea Yanga ligi kuu.
“Kama hawatafika basi haraka tutalifikisha suala hilo Fifa kwani beki huyo ni mchezaji halali wa Simba,” alisema Rage.
No comments:
Post a Comment