Sunday, August 12, 2012

RECHO ABANWA SKENDO YA KUVAA NUSU UTUPU, AJITETEA


WIKI hii tunaye mwigizaji Rachel Haule ‘Recho’ ambaye anajibu na kufafanua juu ya maswali ambayo mmemuuliza.
Kuhusu rushwa ya ngono
Ulikuwa unapenda sana kuigiza lakini nafasi ulikuwa hupati, kwenye filamu yako ya kwanza kushirikishwa nasikia ulitoa rushwa ya ngono. Ni kweli? Issa Chongono, Tanga, 0714455748
RECHO: Siyo kweli, aliyenitoa ni mwanamke mwenzangu.
Huyu anamjua
Nakufahamu Recho, unaishi Sinza maeneo ya uwanja wa mpira karibu na Shule ya Grace. Msomaji, 0719476653
RECHO: Ni kweli.
Huyu anaomba urafiki
Recho nakuzimia jinsi ulivyo na umbo zuri, naomba uwe rafiki yangu. Salim Liundi, Dar, 0658110395
RECHO: Asante, karibu.
Anajitahidi
Recho unajitahidi kwenye kuigiza lakini umbo lako ndilo linakubeba zaidi, jipange. Cassian, 0655202202
RECHO: Asante.

Kuhusu kuvaa nusu uchi
Recho una kipaji lakini nataka kujua, je, bila kuvaa nguo za kuonesha mwili wako muvi haiuziki? Queen Materu,  0653436603
RECHO: Nimezoea kuvaa nguo fupi tangu nikiwa mtoto.

Kuhusu yeye
Dada Recho nakukubali kwa kazi yako nzuri, nataka kujua wewe ni kabila gani, una miaka mingapi na umezaliwa wapi? Ramadhani Khamisi, Tanga, 0717236195
RECHO: Mimi ni Mngoni, nina miaka 24, nimezaliwa Dar.

ANAIFUNDISHA NINI JAMII?
Wewe kama msanii kioo cha jamii, unafundisha nini jamii ukivaa nguo nusu uchi? Mama Elvis, Dar, 0656334307
RECHO: Sifundishi jamii kuvaa nguo fupi ila ni kwa kile ninachoigiza.

Atulie na Saguda
Ukweli unajitahidi sana, kaza buti na kama upo na Saguda tulia uepuke skendo. Zulphathy, Dar, 0719777492
RECHO: Asante.

Idadi ya wanaume
Recho umetembea na wanaume wangapi na je, umewahi kupima Ukimwi? Baba Sapnah, Katavi, 0718296327
RECHO: Sijatembea na wengi na Ukimwi nimepima, sina.

Ana shepu nzuri
Una shepu nzuri dada, nini matarajio yenu na Saguda? Gloria, 0719603656
RECHO: Kuoana.

Akihongwa gari je?
Recho hebu kuwa muwazi kwa hili, tafakari hali ya kazi, mapenzi na maisha ya kesho, jinsi ulivyo mzuri ukihongwa Rav4 umsaliti mpenzi wako utakataa? John, Dar, 0752535336
RECHO: Mimi siamini kama maisha yangu ni Rav4.

Ana watoto?
Recho nakufagilia wewe mkali halafu huna skendo, je, una watoto wangapi? Clara Ritte, Arusha, 0766665002
RECHO: Sina.

Yeye na Steve
Wewe na Steve Nyerere mna ukaribu gani maana filamu nyingi uko naye? Timilai Shemalamba, Tanga, 0653702100
RECHO: Steve ni bosi wangu.

Eti alitoka na HemedY
Recho nilisikia ulishawahi kutoka kimapenzi na Hemedy (Suleiman). Charles Mhando, Mwanza, 0759022399
RECHO: Siyo kweli.

Ana muda gani kwenye gEmU?
Una muda gani kwenye filamu na umecheza filamu ngapi ambazo ni za kwako mpaka sasa? Emmanuel Bernard, Arusha, 0756377286
RECHO: Nina mwaka mmoja na nimecheza filamu mbili za kwangu.

Aheshimu vyombo vya habari
Rachel wewe ni msanii na usanii siyo kuuza sura bali ni kuelimisha jamii, endelea kuheshimu vyombo vya habari mwisho ndivyo vitakavyokufanya utoke. Juma, Moro, 0716110028
RECHO: Sawa, asante.

Huyu anaomba ushauri
Dada Recho napenda uigizaji wako na mimi napenda niwe kama wewe, nitafanyaje ili niwe kama wewe? Msomaji, 0762 732514
RECHO: Nenda kwenye vikundi vya sanaa.

Yeye na Prof Jay
Recho una undugu na Prof Jay? Je, ni kweli sanaa haihitaji elimu, una mpango gani na elimu ya sanaa? Nakukubali ongeza bidii. Mr. Kucha, Dar, 0752535336
RECHO: Hapana siyo kweli, mpango wangu ni kujiendeleza zaidi na elimu ya sanaa.

Nje ya uigizaji
Dada Recho nakukubali sana, nje ya uigizaji unajishughulisha na kazi gani na nini malengo yako ya baadaye? Godfrey, Korogwe, 0656071565
RECHO: Mfanyabiashara, malengo yangu ya baadaye ni kuwa msanii wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment