Stori: Erick Evarist na Gladness Mallya
TAARIFA za ndani zilizotua juu ya dawati la Ijumaa Wikienda zinadai kuwa mwigizaji wa kitambo ndani ya Bongo Movies, Nuru Nassor ‘Nora’ ana kitumbo ndii.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Nora, baada ya kukaa ndani ya ndoa kwa zaidi ya miaka miwili na mumewe Masoud Ally ‘Luqman’ bila kupata mtoto, hatimaye sasa amenasa.
Huyu hapa sosi: “Nimepita pale saluni kwa Nora, Tabata Segerea nikampiga na picha hizi hapa kama hamuamini ngoja niwaletee mzione wenyewe mbona tumbo linaonekana kabisa? Kwa taarifa yenu yupo pregnant (mjamzito).”
Baada ya kunyetishiwa madai hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni na taarifa hizo zilipozidi kuenea kama moto wa kifuu ndipo likamtafuta Nora ambapo aliishia kucheka na kusema:
“Hahahahaha nani huyo kawaambia? Mh! Mna mambo! Mimi sina jamani, ila kama wanasema hivyo ni wao na kwa vile ni jambo la heri basi inshaallah!”
No comments:
Post a Comment