Monday, August 13, 2012

VITU MUHIMU VYA KUFAHAMU KAMA ULIMIS BAJETI YA WIZARA YA ELIMU BUNGENI AUG 13.


0
.
Ishu ya Serikali kuendelea kutegemea fedha za nje kwenye kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo imeendelea kujitokeza ambapo sasa ni wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kutangaza kutumia bilioni 74 kutoka kwa wahisani wa kimaendeleo kwenye bajeti yake.
Wakati anawasilisha bajeti ya wizara yake Waziri Dr Shukuru Kawambwa amesema kati ya shilingi bilioni 92.5 zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wizara hiyo, ni bilioni 18.5 tu ndizo fedha zitakazotumika kutoka vyanzo vya ndani huku hizo bilioni 74 zikitoka kwa wahisani.
Akizungumza bungeni, Waziri Kawambwa amesema “Mh Spika naliomba bunge lako tukufu liidhinishe makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya elimu ya mafunzo ya ufundi ya jumla ya shilingi bilioni mia saba ishirini na nne, milioni 471 na laki tisa elfu 37 kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kuiwezesha wizara kutekeleza majukumu yake”
Umeaza nini baada ya kusoma hayo maelezo, unaweza kutoa mchango wako kwa kucomment..

No comments:

Post a Comment