Wednesday, August 15, 2012

KLABU YA WAOGELEA UCHI YAKAMIA KUVUNJA REKODI

Wanachama wa kundi la Secret Cinema wakijiachia katika Bustani ya Cornbury, Oxfordshire,  nchini Uingereza.
KUNDI la siri liitwalo Secret Cinema, hivi majuzi lilikutana katika Bustani ya Cornbury, Oxfordshire,   nchini Uingereza,  kwa ajili ya kuogelea uchi.
Waogoleaji hao ambao walikuwa wamekutana kwa mara ya kwanza kufuatia mawasiliano miongoni mwao, walijibwaga katika maji ya baridi asubuhi ya saa mbili Jumamosi iliyopita katika ziwa moja karibu ili kujaribu kuvunja rekodi kwa kufanya ujasiri huo.
Tukio hilo pia liliashiria kuanzishwa kwa Klabu ya Siri ya waogoleaji ambao watakuwa wakiogelea uchi kila mwezi.
Mwasisi wa kundi hilo ambalo litajulikana kama Future Cinema and Secret Swimming, Fabien Riggal, aliuambia mtandao wa Wired.co.uk kwamba wazo hilo limepokelewa kwa furaha na wahusika wote waliohudhuria.
Hata hivyo, haijafahamika iwapo hafla hiyo ilivunja rekodi ya watu kuogelea uchi katika maji ya baridi asubuhi.

No comments:

Post a Comment