Mkuu wa Polisi Wilaya ya Magomeni akiongea na wanafunzi walioandamana akiwasihi warudi shuleni kwao.
Baadhi ya maofisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni waliofika kuwatambua wanafunzi hao na shule wazikotokea.
Kikosi maalum cha polisi kutoka ofisi ya Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kikifuatilia nyendo za mgomo huo.
MGOMO wa walimu nchini umeendelea kutikisa sehemu mbalimbali likiwemo
jiji la Dar es Salaam ambapo hali si shwari na wanafunzi wameendelea
kuandamana kudai haki ya wao kusoma.Mtandao huu umetembelea sehemu mbalimbali za jiji na kubaini kwamba shughuli za masomo bado zimesimama karibu sehemu zote za jiji, hali ambayo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Lugimbana alikiri kwa kusema “hali bado ni tete.”
(PICHA: HARUNI SANCHAWA, GPL)
No comments:
Post a Comment