Sunday, August 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra jana Agosti 11, 2012 baada ya kumtembelea na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa juzi. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra jana Agosti 11, 2012 wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama mananasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa mananasi yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shamba la Bomarts Farms Ltd katika kijiji cha Dobro katika eneo la Nsawam nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya bluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo, Mhe. Kwesi Ahwol. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd, Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda. (PICHA NA IKULU)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana Agosti 11, 2012 baada ya  kumtembelea na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa juzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra jana Agosti 11, 2012  wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama mananasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha  Bomarts Farms Ltd katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa mananasi yanayolimwa  kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shamba la Bomarts Farms Ltd katika kijiji cha Dobro katika eneo la Nsawam  nje kidogo ya jiji la Accra jana Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya bluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo, Mhe. Kwesi Ahwol.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya  mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd, Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda.
(PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment