Wednesday, August 1, 2012

DUDE ADAIWA KUMTAPELI MWIMBA INJILI


Na Erick Evarist
STAA wa muvi Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ (pichani) amekwaa skendo ya kutapeli ngawira za Kibongo kiasi cha shilingi milioni 4 kutoka kwa mdau mmoja wa sinema, Felix Ilomo.
Kwa mujibu wa Ilomo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili na mkazi wa Keko jijini Dar, alimkabidhi Dude kiasi hicho cha fedha ili amsimamie kushuti wimbo wake akimuamini yeye ni mzoefu katika masuala ya video.
“Nilimwamini Dude atanisaidia, nikamkabidhi shilingi milioni 4 ambazo alisema zinahitajika ili niweze kurekodi wimbo wangu wa Kwa Neema Yako Yesu. Fedha hizo nilimpa toka mwanzoni mwa mwaka huu lakini kila kukicha sioni video wala nini, alidai tungeshuti katikati ya Januari, nikimuuliza ananipiga kiswahili hadi leo. Nimechoka lazima nimchukulie hatua za kisheria,” alisema Ilomo.
Dude alipotafutwa kwa njia ya simu na kusomewa mashitaka, alisema: “Siwezi kumtapeli bwana, nashindwa kuelewa kwa nini anakosa imani wakati nimeshamwambia asubiri jamaa arudi tutarekodi.”

No comments:

Post a Comment