Thursday, August 2, 2012

HILI NDIO JIBU LILILOTOLEWA KWA MSECHU BAADA YA KUMKOSOA HUYU MSHINDI WA TUSKER, AMEMJIBU!



.
Exclusive kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Aliyewahi kuwa mshindi wa Tusker Project fame All Stars Mtanzania Peter Msechu alifunguka ya moyoni kwa kusema mshindi wa pili wa Tusker Project Fame 2012 Mkenya Doreen hakustahili kushinda hiyo nafasi.
Alisema “Doreen hakustahili kuwa mshindi kwenye nafasi ya pili kwa sababu hana uwezo mkubwa wa kuimba na kuperform kama Jackson wa Rwanda ambae alishika nafasi ya tatu, watu wengi sana wamelalamika hivyo hata mimi sijaridhishwa kwa sababu alietakiwa kushika nafasi ya pili ni Jackson alafu Doreen ndio alitakiwa kuwa wa tatu”
Baada ya maneno hayo ya Msechu, Doreen alipata nafasi ya kuzungumza na millardayo.com Exclusive na kusema “maoni yake ni maoni yake Msechu na yeye ni mtu mmoja kati ya watu milioni walionipigia kura, kuna watu wengi sana wanaonikubali hivyo maoni yake hayaniumizi chochote namwambia tu tukutane kwenye industry ndio nimeingia rasmi, tutaonana”

No comments:

Post a Comment