Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, viongozi wa umoja huo kwa pamoja walisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo imekuwa ni kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao,” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Jacobo Steven ‘JB’, alisema serikali inapaswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kufanya kazi zao kwa nguvu zote.
Kwa upande wake Meneja wa Usimamizi kutoka TRA, Msafiri Ndimbo, alisema mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari mwakani hasa baada ya serikali, kupitia bunge, kukubaliana kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.
No comments:
Post a Comment