Monday, August 20, 2012

SIMBA YATELEKEZA FAMILIA YA MAFISANGO

Uongozi wa simba unalaumia kwa kosa la kutelekeza familia ya  Marehemu mafisango kwakutolipia kodi ya sehemu ambayo aliokuwa akikaa mcheza wao patrick mafisango. mpaka imepelekea kutolewa vitu nje ya nyumba na kumpisha mpamngaji mwengine.akiongea na mwenye nyumba mdaku wetu alisema bobani na kesi walimwambia kwamba wangepeleka pesa kwa ajili ya malipo ya hiyo sehehmu hili ndugu hao wamafisango waendelee kukaa hapo. lakini mpaka dakika ya mwisho kesi akipigiwa hapokei simu na akazima kabisa. bobani alipokea simu akasema atakuja kulipia jioni tangu tarehe 8 mpaka leo. nimeamua kuvitoa vitu vya marehemu nje hakuna mtu yeyote aliejitokeza sio mchezaji wala kiongozi wa simba. mdaku wetu pia aliongea na kiongozi wa simba akasema" wao kama simba waliingia mkataba na marehemu mafisango nawala hawakuingia na hao ndugu na marafiki wa mafisango ambao wanakaa hapo.  hivyo sisi kama simba tunakaa na kujadili jinsi yakuwasaidia mwisho wa siku tutatoa jibu linaloeleweka. ndugu hao wamafisango wamesema" wanachoomba wao nikurudishwa vitu vya marehemu mafisango  nchini kwao rwanda tu basi.  kwanini washindwe kutusaidia au kwasababu ndugu yetu ameshafariki?alilalamika rwandizi mmoja wa ndugu wa mafisango.
 Timu ya simba ikiwa na masisango aliezungushiwa kiduara
 Safari ya mwisho ya marehemu mafisango akiagwa na watanzania leaders club
Gari alilopata nalo ajali marehemu masisango mpaka kupekekea kifo chake maeneo ya keko dsm.

No comments:

Post a Comment