Wednesday, August 29, 2012

MAREHEMU BABA WA SHIGONGO ALIVYOAGWA NA WAKAZI WA DAR

Mwili wa mzee James Bukumbi ukiwasili Kijitonyama kwa gari maalum.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, akipokea jeneza la mwili wa baba yake.
Mama yake Shigongo, Asteria Kapera (kushoto) akiwa mwenye masikitiko.
Jeneza likiwa nyumbani Kijitonyama.
WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam leo walifurika nyumbani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, kwa ajili ya kuuaga mwili wa baba yake mzazi, mzee James Bukumbi, aliyefariki jijini Dar es Salaam Agosti 25 mwaka huu.  Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wa aina mbalimbali ilifanyika nyumbani kwa Shigongo, eneo la Kijitonyama, jijini.

TAARIFA KAMILI KUHUSU DIDIER DROGBA KUONEKANA TENA CHELSEA.


2
.
Mtandao wa Give me football umeripoti kwamba Mkali wa soka Didier Drogba ambae baada ya mkataba wake na Chelsea kuisha alisain dili jipya na club ya Shenhua ya China, amerudi na kuonekana kwenye mazoezi na Chelsea.
Katika kipindi hiki cha mapumziko kwenye msimu wa soka China, Drogba amerudi London kuisalimia familia yake lakini pia alionekana kwenye uwanja wa mazoezi na Chelsea.
Give me Football wamezidi kutiririka kwamba kuna uwezekano huo ndio ukawa mwisho wa Drogba kuichezea Shenhua baada ya kugundulika kwamba club hiyo inahangaika kutafuta pesa za kuendelea kuwalipa wachezaji wake kutokana na pesa nyingi kutolewa kwa mishahara ya Drogba na Anelka.
Kutokana na club hiyo kuwa na tatizo la kifedha kwa sasa upo uwezekano mkubwa wa Drogba na Anelka kuuzwa kwenye club nyingine ili angalau hizo pesa zisaidie kuiokoa Shenhua, kutokana na hilo pia kwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa Drogba kurudi kuichezea Chelsea kama itakubali kuilipa Shenhua.

PICHA ZA INTERVIEW YA MILLARD AYO NA CMB PREZZO ON CLOUDS TV.


6
Ni interview ambayo itaonekana Clouds TV, hii ni wakati Prezzo alipofika Moshi kwa ajili ya kufanya show ya Serengeti Fiesta.
Baadhi ya aliyoyaongea ni pamoja na kwenda Nigeria kuwaomba msamaha Wanigeria kuhusu Goldie waliekua pamoja kwenye Big Brother.
.
.
.
Dj wa Prezzo ambae pia huwa ni Dj wa Ay, Athur akipita pembeni yetu.

KILICHOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO AUGUST 29 KWENYE UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS!


3
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

PICHA ZA AJALI NYINGINE YA LORI KARIBU NA CHALINZE.


0
Sikuweza kupata details kamili za hii ajali lakini ni ajali ya nne ya Lori niliyokutana nikitokea Tanga kuja Dar es salaam, hapa ni karibu na Chalinze na ni sehemu ya tambarare kabisa.
Kumekua na mfululizo sana wa ajali za magari makubwa katika kipindi hichi.

HUYU NDIO MREMBO WA KITANZANIA ANAESHINDANIA MISS EAST AFRICA BELGIUM.


3
.
.
.
Jina lake ni Juliana Pierre mtanzania ambae yuko kwenye list ya warembo wanaolitaka taji la Miss East Africa Belgium 2012 ( representing Tanzania), mwenye nguvu ya kumuweka kwenye nafasi ya ushindi ni wewe pekee kwa kulike page yake ya facebook… please tumsupport mtu wetu kwa kukopi na kulike hiyo page yake ya facebook hapo chini, mimi nimeshalike tayari….
http://www.facebook.com/JulianaPierreFinalisteMissEastAfricaBelgium2012

EXCLUSIVE: HII NDIO PETE YA UCHUMBA ALIYOVISHWA MWIGIZAJI AUNT EZEKIEL!

s
7
Huu ni mkono wa Aunt Ezekiel na hiyo ndio pete aliyovishwa na mchumba wake Dubai.
Aunt Ezekiel kwenye nterview na Millard Ayo.
Stori kamili ni kwamba bado mpaka sasa movie star wa Tanzania Aunt Ezekiel hajaolewa ila pete ya uchumba tayari ameshavalishwa kwenye party iliyofanyika huko Dubai, ndoa ni mwezi november na itafanyika hukohuko Dubai.
Aunt amesema aliemvisha pete ya uchumba sio mwigizaji wala mtu maarufu wa Tanzania kwa sababu huwa hapendi kuwa kwenye mapenzi na staa, mumewe mtarajiwa ni Sunday Demonte…. na anauhakika huyu wa sasa atakua tofauti na mwanaume aliekua nae 2008/2009 aliekua anampiga na kumnyanyasa kila siku.
Aunt amesema ndoa yake itakayofungwa Dubai itahudhuriwa na watu 100 tu, amezungumza pia mengine kuhusu kubadili dini na kufata dini ya mume, kuhamia Dubai pamoja na ishu nyingine…. utaendelea kupata info nyingine hapahapa millardayo.com pamoja na kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM.