Kikosi cha Yanga kilichoanza mechi ya leo.
TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kuingia Fainali ya Michuano ya Kombe la
Kagame leo baada ya kuilaza timu ya APR ya Rwanda bao 1-0 kwenye mchezo
wa Nusu Fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bao la
Yanga limefungwa na mchezaji Hamis Kiiza katika muda wa nyongeza baada
ya dakika 90 kumalizika 0-0. Kwa matokeo haya, Yanga itakutana na Azam
FC katika fainali itayochezwa Jumamosi Julai 28, 2012 katika Uwanja wa
Taifa.
No comments:
Post a Comment