Saturday, July 21, 2012

agnes anywa sumu

Na:Imelda Mtema
MUUZA sura anayetamba kwenye video za Kibongo, Agness Jerald ‘Masogange’ juzikati alinusurika kuaga dunia baada ya kuchanganya pombe na dawa aina ya Cephalaxin kutokana kuudhiwa na mpenzi, Risasi Jumamosi lina habari kamili.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Masogange aitwaye Janneth asubuhi ya siku ya tukio, Agness alimpigia simu na kumtaka afike nyumbani kwake kwa kuwa tumbo lilikuwa likimsumbua.
Hata hivyo, Janneth alidhani rafiki yake huyo alikuwa akimtania, kwa kufikiria kuwa alikuwa akimtaka tu afike nyumbani kwake na hakuwa na tatizo lolote.…
Na:Imelda Mtema
MUUZA sura anayetamba kwenye video za Kibongo, Agness Jerald ‘Masogange’ juzikati alinusurika kuaga dunia baada ya kuchanganya pombe na dawa aina ya Cephalaxin kutokana kuudhiwa na mpenzi, Risasi Jumamosi lina habari kamili.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Masogange aitwaye Janneth asubuhi ya siku ya tukio, Agness alimpigia simu na kumtaka afike nyumbani kwake kwa kuwa tumbo lilikuwa likimsumbua.
Hata hivyo, Janneth alidhani rafiki yake huyo alikuwa akimtania, kwa kufikiria kuwa alikuwa akimtaka tu afike nyumbani kwake na hakuwa na tatizo lolote.

Jananeth alizidi kueleza kuwa baada ya muda alipigiwa tena simu na Agness huku akilia ndipo alipohisi kuwa kulikuwa na kitu, akaamua kukodi teski kwa ajili ya kumuwahi.
“Nilipofika nyumbani kwake nilikuta amejifungia kwa ndani, hivyo ikabidi kuvunja mlango, nilipofanikiwa kuingia nilimkuta akiwa hoi,” alisema Janneth.
Janneth alisema kuwa baada ya kuvunja mlango alimkuta Agness akiwa amelala karibu na chooni na pembeni yake kukiwa na chupa ya pombe na pakti ya dawa.

“Nilikwenda dukani na kumnunulia maziwa na kumnywesha kwa kuwa nilihisi atakuwa amechanganya dawa na pombe, kisha nikamkimbiza katika Hospitali ya Mama Ngoma kwa ajili ya matibabu.”
Baada ya kupata taarifa hizo na kuambiwa kuwa Agness alikuwa amesharudi nyumbani kwake, mwandishi wetu alimfuata na kumkuta akiwa amejilaza nje ya nyumba yake, hapohapo akamdodosa kwa maswali:
Risasi: Kuna hisia kuwa umekunywa pombe na kuchanganya na dawa?

Agness: Ni kweli.
Risasi: Ulifanya kwa kudhamiria au?
Agness: Kwa kweli nilidhamiria.
Risasi: Kisa hasa ni nini?
Agness: Ni mapenzi tu yanitesa.
Risasi: Vipi umesalitiwa au?
Agness: We acha tu,nitakueleza nikiwa vizuri.
Bado gazeti hili litaendelea kumdodosa Agness kisa kilichomfa kufikia hatua hiyo, fuatilia.

No comments:

Post a Comment