Tuesday, July 24, 2012

RECHO: NIPO KWENYE MFUNGO


Rachel Haule ‘Recho’.
Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ amefunguka kuwa hana mpango wa kujichanganya katika starehe mwezi huu wa Ramadhan kwa sababu anafunga na kutubu dhambi zake.
Akichezesha taya na Tollywood Newz, Recho alisema atautumia muda wake mwingi kushinda nyumbani akiomba dua kwa Mungu wake ili amsamehe makosa yake yote aliyoyatenda huku akifunga kama wafanyavyo Waislam ingawa yeye ni Mkristo.
“Mama yangu ni Muislam, baba ndiyo Mkristo. Ninauheshimu mwezi mtukufu kwani nimezungukwa na ndugu wengi wa imani hiyo, hata mavazi ninayovaa sasa hivi yanapendeza kwa kweli nimeacha kuvaa vimini mpaka mwezi utakapoisha,” alisema Recho.

No comments:

Post a Comment