Tuesday, July 24, 2012

WOLPER NA UWOYA WAPANANISHWA TENA



Jacqueline Wolper na  Irene Uwoya.
Stori: Shakoor Jongo
TAKRIBANI siku 15 tangu wasanii Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyeinye’ na Jacqueline Wolper Masawe wapatanishwe na kumaliza tofauti zao, Ijumaa Wikienda linakuwa la kwanza kukujuza kuwa naye Irene Pancras Uwoya na Wolper wamepatanishwa.
Mchakato huo wa kumaliza tofauti na kuanza ukurasa mpya ulianza takribani miezi miwili iliyopita hadi Julai 18, mwaka huu, ulipofikia tamati pale Samaki-Samaki, Mlimani City jijini Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini kilichohusika na upatanisho huo, kilisema siku hiyo ya Jumatano wiki iliyopita, ndiyo ulikuwa mwisho wa mastaa hao wawili kutofautiana.
“Njoo fasta hapa Samaki-Samaki, yule Daudi Kipunguni mliyemwandika kanaswa na Sylvia Shally anawapatanisha Uwoya na Wolper.
IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kumwagiwa ‘upupu’ huo, Ijumaa Wikienda lilitia timu Mlimani City lakini kutokana na foleni za jijini Dar halikuwakuta.
Baada ya kuwakosa, paparazi wetu alimwendea hewani shuhuda wa tukio hilo ambaye aliendelea kuthibitisha kuwa ni kweli wawili hao wamesuluhishwa.
SH. MILIONI 7 ZATUMIKA
Ijumaa Wikienda lilipododosa kuhusu mchakato huo ulianza lini na kama kuna gharama zozote zilizotumika, shushushu huyo alidai kuwa alimsikia Daudi (mpatanishi) akisema kuwa zoezi hilo lilichukua muda mrefu na kama ni suala la gharama siyo chini ya Sh. milioni 7.
WOLPER ANASEMAJE?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kuhusu ishu hiyo, mbali na kukiri kukutana na Uwoya Mlimani City, Wolper alifunguka kuwa walikutana mahali hapo kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana.
“Tumemaliza tofauti zetu, sasa ni kazi tu ili kuelimisha jamii, mabifu hayana nafasi tena,” alisema Wolper.
UWOYA KAMA KAWA
Uwoya kama kawaida yake hakupatikana kwa kuwa siku hizi hana namba ya kumpata muda wote kwani zile za zamani zote hazipatikani.
WEMA ATIA NENO
Naye staa asiyechuja, Wema
Sepetu aliposikia upatanisho wa Wolper na Uwoya alikuwa na haya ya kusema:
“Sasa naamini mashabiki wetu watapata ladha yetu ambayo inawezekana waliipoteza siku nyingi, nimefurahi sana.”
KWANI TATIZO LILIKUWA NI NINI?
Miezi kadhaa Wolper na Uwoya waliingia kwenye vita nzito kisa kikiwa ni mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Ababuu ambaye alikuwa mchumba wa Wolper kabla ya baadaye kuwepo kwa tuhuma kuwa Uwoya alimkwapua.

No comments:

Post a Comment