HII NDIO TAARIFA YA WAZIRI KUJIUZULU ZNZ KUTOKANA NA AJALI YA MV SKAGIT.
Posted: 23rd July 2012 by MillardAyo in NewsBaada ya kujiuzulu nafasi yake imechukuliwa na RASHID SEIF SULEIMAN ambae ni mwakilishi wa jimbo la Ziwani mkoa wa kusini Pemba.
Mwandishi Khaleed kutoka Zanzibar amesema “ni kweli nimepata taarifa za kujiuzulu kwa Waziri huyo, aliandika barua ya maombi ya kujiuzulu kwa Mh Rais na barua hiyo leo ndio amejibiwa rasmi, alishajiuzulu toka saa 12 leo jioni ambapo wananchi wa Zanzibar walimuandama sana ndio kisa cha kujiuzulu”
“Wananchi walifurahi sana kwa kujiuzulu kwake kwa sababu hana umuhimu kwenye utendaji kazi wake, kila mtu kafurahi sana na mpaka sasa zinafanywa sherehe mbalimbali kwa kujiuzulu kwa waziri huyo, kulikua kuna vurugu la uamsho lakini mpaka sasa tunamshukuru Mwenyezi Mungu Zanzibar hali ni shwari hakuna vurugu ya aina yoyote wala barabara kuchomwa na kupangwa mawe” Khaleed.
No comments:
Post a Comment