Saturday, July 21, 2012

HUYU NDIO MCHUMBA WA THE GAME ALIEKUA AFUNGE NAE NDOA.

The Game na Tiffney Cambridge.
Wiki chache baada ya Rapper THE GAME kutangaza kwamba soon atafunga ndoa na mwanamke aliemzalia (Tiffney Cambridge), rapper huyo ghafla ametangaza kuahirisha kufunga hiyo ndoa.
Kupitia page yake ya twitter yenye zaidi ya watu milioni moja na elfu hamsini, The Game member wa zamani wa G UNIT ambae alishawahi kuja kupiga show Nairobi Kenya na kushare stage na Jua Cali, aliandika kwamba harusi imefutwa.
Kasema hiyo imetokana na kosa alilolifanya yeye na sio huyo mama watoto, ambapo ametoa msisitizo kwa wanaume wanaopata bahati ya kuwa na wanawake wenye mapenzi ya dhati kama huyo, wahakikishe hawawaachii.. wawape happy.
Japo hakuna sababu za wazi za kufutwa kwa harusi hiyo, Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali wa SO SO FRESH ya CLOUDS FM aliongea kwenye XXL kwamba inaaminika Game kaahirisha harusi kwa kuogopa kisasi ambacho angeweza kulipizwa na mshkaji ambae wamekua na beef la muda, mshkaji ambae Game na watu wake 14 walijikusanya na kwenda kumpiga.
.
.
.
The Game na watoto wake, sio wa mama mmoja.
Mtoto mwingine wa The Game.

No comments:

Post a Comment