Thursday, July 26, 2012

PICHA ZA MECHI ZA YANGA NA AZAM UWANJA WA TAIFA JULY 26 2012.

1
.
APR na YANGA.
Said Bahanuzi akiwa amembeba Hamis Kiiza baada ya kufunga goli pekee la Yanga dhidi ya APR ya Rwanda.
.Wakati-wa-mapumziko-mechi-ya-Yanga-na-Vita-Kocha-wa-Yanga-Tom-Saintfiet-alimuita-kocha-wa-Azam-Stewart-Hall-kumuelekeza-mambo-na-kipindi-cha-pili-Azam-ikatoka-nyuma-kwa-1-0-na-kushinda-2-1
.
AZAM FC VS AS VITA YA CONGO DRC.
Azam akiwa anashangilia goli kwa mashabiki wa Yanga baada ya kufunga goli la pili huku la kwanza likiwa limefungwa na John Bocco na hivyo kuchukua ushindi wa 2-1 dhidi ya AS VITA ya Congo DRC.
.
John Boko na wenzake wakishangilia goli. (Picha zote zimepigwa na bongostaz.blogspot.com )
Hapa ni kwenye ubalozi wa Tanzania Uganda, kama hufahamu chochote kuhusu hii stori ya Chameleone na Big Boss Erick Shigongo, nenda kwenye post zilizopita.
.
(Picha zote kutoka kwa Bill The African)

HIZI NDIO STORY KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO JULY 26

Posted: 26th July 2012 by MillardAyo in News
0








9
Wabongo wengi hawakumjua sana mwimbaji wa R’n'B Frank Ocean wa Marekani lakini wakamfahamu zaidi baada ya kuandika barua na kukiri hadharani kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja (Shoga) na hata kwenye album yake mpya kuna nyimbo za mapenzi kamuimbia mwanaume mwenzake, sasa leo nimefanikiwa kupata Video mpya ya Rapper Mmarekani mweusi ambae amekua rapper wa kwanza mimi kumuona akikubali hadharani kwamba yeye ni shoga.
Nimejaribu kuchek video yake kiukweli naona nisiongee chochote, ila nikupe nafasi na wewe umtazame kwenye hizi dakika mbili na sekunde 49 alafu baada ya hapo ndio nisikie niyasome maoni yako.

Mpaka sasa hiyo video imetazamwa na zaidi ya watu 2400, mara ya mwisho nimeichek kulikua na watu 27 walioipenda na wanne hawajaipenda.
Hili ni jipya kwa 2012, Rapper huyu aitwae  Le1f  ameamua kuweka wazi kwamba ni rapper shoga lakini hakuna rap ya mashoga, ni ya watu wote.
Unaweza kulike na kutweet hii stori ili na wenzako waione.
8
Jose Chameleone akiperform wakati wa Usiku wa Matumaini, tamasha lililoweka Historia ya burudani 2012 kwa kuandaliwa na Global Publishers wakishirikiana na wadau wengine.
Kama kumbukumbu zako zipo fresh, muda mfupi baada ya Jose Chameleone kumaliza show yake Uwanja wa taifa July 7 2012 na kufanya kama walivyokubaliana kwenye mkataba, siku mbili baadae stori gazetini ziliandikwa kwamba mwimbaji huyu staa wa Uganda ameshindwa kurudi kwao kutokana na Passport yake ya kusafiria kushikiliwa na Eric Shigongo C.E.O wa Global Publishers walioandaa show hiyo kutokana na kumdai pesa ambazo ilidaiwa alishawahi kulipwa kipindi cha nyuma kuja kufanya show Tanzania lakini hakutokea.
Pamoja na hati yake ya kusafiria kuzuiliwa na Erick Shigongo, aliweza kusafiri kurudi kwao… sasa baada ya kuwa kimya kidogo…… hiki ndicho alichoandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu hiyo ishu.
Kwa ufupi ni kwamba Jose Chameleone amemlalamikia Big Boss Erick Shigongo kuhusu kuendelea kuishikilia Passport yake wakati meneja wake Chemeleone hakuhusika kuchukua hizo dola za Kimarekani 3500 zinazodaiwa kupokelewa na Meneja wa Chameleone kwa ajili ya show iliyopangwa siku nyingi kidogo.
Chameleone amesema aliporudi Uganda alifanikiwa kumkamata na kumpeleka polisi George, mtu ambae ndio anadaiwa kuzichukua hizo pesa akijidai ni meneja wa Chameleone lakini baadae akaachiwa huru ambapo baada ya kuona hivyo ilibidi Chemeleone aende kwa balozi wa Tanzania Uganda ili kupata msaada lakini hakufanikiwa.
Amesema wakati passport yake ilipozuiliwa na Erick Shigongo alikwenda kwenye ubalozi wa Uganda Tanzania na ndio uliomsaidia kumpa Document zilizomuwezesha kurudi nyumbani, kwa sasa amepata mialiko ya shows South Africa, England, Belgium, Norway, Sweeden, Canada n.k lakini hajui itakuaje na anahitaji ushauri kuhusu Erick Shigongo ambae ameshikilia Passport yake kwa zaidi ya mwezi mmoja.
.
.

No comments:

Post a Comment