TANGAZO LA VIPINDI VYA MASOMO KIDATO CHA TANO NA SITA
Makamu wa Rais |
Shirika la Elimu
Kibaha kupitia Idara yake ya Huduma za Elimu ambayo inasimamia shule ya
sekondari Kibaha, shule ya wasichana Kibaha na Shule ya Sekondari Tumbi,
ambazo kwa pamoja zinatoa elimu bora ya sekondari kwa ngazi za kidato cha nne na sita. Mwaka
2004, Shirika lilianzisha masomo ya jioni katika Shule ya Sekondari
Tumbi, mpango unaojulikana kama “SOGEA” kwa wanafunzi wanaojiandaa na
mitihani ya Kidato cha Nne na mtihani wa Maariifa (QT).
Katika kuongeza wigo
wa elimu, Shirika la Elimu Kibaha linapenda kuwatangazia wananchi wote
kuwa, kuanzia mwezi April 2012, litaanza kutoa mafunzo ya jioni ya
kidato cha tano katika shule ya sekondari Kibaha kwa michepuo ifuatayo:-
* ECA * HGE * EGM * HGL * HGK * HKL
Vipindi vitaanza saa
09:00 alasiri hadi saa 1:00 jioni Jumatatu hadi Ijumaa . Kujiandikisha
fika Shule ya Sekondari Kibaha saa 03:00 asubuhi hadi saa 09:00 alasiri
siku za Jumatatu hadi Ijumaa.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Msajili wa Wanafunzi,
Shule ya Sekondari Kibaha,
S.L.P. 30053,
Simu: +255 714 920 110
+255 757 332 233
No comments:
Post a Comment