Wednesday, June 20, 2012

Mnyika atimuliwa

MNYIKA ATIMULIWA BUNGENI KWA KUMDHIHAKI RAIS

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika akiingizwa na askari wa bunge kwenye gari baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe nje ya viwanja vya bunge baada yambunge huyo kugoma kufuta kauli yake kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
BUNGE jana lilichafuka tena baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kauli ambayo ilisababisha Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe bungeni.

Mnyika alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13, ambapo alieleza kuwa analazimika kusema Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, wabunge ni wazembe na nchi imefika hapa ilipo kutokana na upuuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM). 

"Mimi nasikitishwa na jambo moja, tumefika hapa kutokana udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa bunge na wabunge na tumefika hapa kutokana na upuuzi wa CCM, nasema hivi nina ushahidi.” 


Kauli hiyo ya Mnyika ndio ilichafua hali ya hewa  bungeni, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi ndipo alisimama na kuomba mwongozo wa Spika.
“Nataka kumbukusha Mnyika, kutokana na kauli zake, kwa kutumia kanuni ya 64 (d) ambayo inaeleza mbunge yeyote hatatumia jina la Rais kwa dhihaka katika mjadala au kulishawishi bunge kwa jambo lolote,” alisema Lukuvi.

No comments:

Post a Comment