Saturday, June 16, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza Afungua Mafunzo ya Afya ya Jamii CHF/TIKA Mkoani Kibaha

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba akizungumza wakati wa kumkarisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza mafunzo hayo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee  (kushoto), akielezea umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), wakati wa ufunguzi wa mafunzo  kwa ajili ya uanzishaji wa  wa Mfuko huo kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani jana.Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza  na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael, akijitambulisha wakati wa mkutano huo
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee  (kushoto), akielezea umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), wakati wa ufunguzi wa mafunzo  kwa ajili ya uanzishaji wa  wa Mfuko huo kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani jana.Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza  na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Diwani wa Kata ya Maili Moja, Kibaha, Andrew Lugano, akitoa shukrani baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, kufungua mafunzo hayo
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha wakiwemo madiwani, wakihudhuria mafunzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (kulia) akiagana na  Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Hamis Mdee baada ya kufungua mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa  wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mjini Kibaha, jana. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba, Mkurugenzi wa Hamashauri hiyo, Jenifa Omole na Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi  wa halmashauri hiyo, baada ya kufungua mafunzo hayo jana.

No comments:

Post a Comment