34
Kuhusu kifo cha
msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga
akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza
mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea
akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es
salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza
hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha
kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya
wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe.