Japokua staa huyu wa single za
‘Nai nai’ na ‘baadae’ hajataka kuweka wazi kwamba ni mamilioni mangapi
yametumika kuitengeneza video yake ya kwanza kuifanya South Africa na ya
kwanza kwa gharama kubwa, amekubali kushea na familia ya millardayo.com
baadhi ya picha zilizopigwa wakati wa utengenezaji wa hii video ya
‘baadae’ huko Johannesburg Afrika kusini.



Picha zinazofata hapo chini ni
kutoka kwenye video fupi ambayo ilitangulizwa kama teaser ya video
kamili ya single ya ‘baadae’ ya Ommy Dimpoz.

Model Tully ambae amehusika kwenye video kadhaa za mastaa wa South Africa pamoja na matangazo mbalimbali ya biashara.

Huyu
ni Luclay mwakilishi wa South Africa kwenye BBA 2011 na hapa aliomba
kumpiga picha Ommy Dimpoz ili akamuonyeshe mpenzi wake kwamba amekutana
na staa kutoka Tanzania.

Ommy
Dimpoz baada ya kwenda shopping alikutana na warembo wa Kikenya ambao
kumbe ni mashabiki zake wakaomba kupiga picha, huyu ni wa kwanza.
No comments:
Post a Comment