Ingawa mara nyingi tumekuwa tukisikia hakuna
usalama wa asilimia miamoja kwenye ulimwengu wa kompyuta,ila kinga ni
bora kuliko tiba. Hebu angalia,wengi wetu tumeweka nondo za kutosha
majumbani mwetu huku tukiwa na lundo la mbwa wakali. Ingawa vyote hivi
sio kama vitawazuia majambazi kukuingilia,ila inaweza kusaidia kuzuia
vibaka wadogowadogo. Kwa mantiki hayo,leo hii tutaangalia njia bora za
kujikinga na kujiweka katika mazingira ya usalama.Binafsi nimeshasahau
mara ya mwisho ni lini kuvamiwa na virusi au minyoo,sio kwakuwa natumia
programu za ulinzi zenye nguuvu saaana au ni bingwa sana kwenye masuala
ya kompyuta hadi virusi vinaniogopa,bali ninafuata kanuni bora za
usalama wa kompyuta ambazo leo hii nitagawana nanyi. Hivyo bila kupoteza
muda hebu tuziangalie kwa mapana yake.
I.Tumia programu unazozihitaji
Wengi tumekuwa wahanga wa matatizo ya kompyuta kwa kujisababishia wenyewe,inawezekana kwa kujua au bila kufahamu.
Kompyuta
nyingi zimekuwa zikiathiria na masuala ya kiusalama sio kutoka nje bali
ndani ya kompyuta husika. Matatizo haya mengi husababishwa na programu
ambazo hazijaandikwa kiusahihi.Chukulia mfano jinsi ukuta wa nyumba
unavyoweza kukuangukia na kuvunja vifaa vyako vya ndani au bati ambalo
halijagongelewa ipasavyo na kuacha tundu kwenye njia ya msumari na
kupitisha maji pindi mvua inaponyesha. Hii ni sawa na hizi programu,kama
programu haijaandikwa ipasavyo inaweza kukusababishia matatizo
mengi.Sio tu kuhitilafiana na mtambo endeshi(OS) wa kompyuta yako na
wewe kuona kama kirusi bali pia inaweza kuacha mianya ambayo wavamizi
wanaweza kutumia kuingia kwenye kompyuta yako.
Je
umewahi kujiuliza kwanini natumia programu hii badala ya ile? Ukuaji wa
teknolojia umesababisha kila mtu kuja na programu yake,kuna zile za
bire,za kugawana na hata zile za bei chee.Sasa sitaki kusema kuwa
programu za bei ya juu ndio bora au zile za bei ya chini ni za kukimbiwa
kama ukoma,ila wewe kama mtumiaji unatakiwa kufanya kautafiti kadogo
kabla ya kuamua kutumia programu fulani. Siku hizi kuna google ambayo
inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kufanya utafiti na kuangalia maoni
ya watumiaji juu ya programu husika.
Kwa kufanya hivi itakusaidia unapata programu ambayo inakidhi mahitaji yako huku ukiwa salama.Mfano mzuri binafsi sijawahi kutumia Windows Vista,kwani kipindi natumia Windows XP na kutaka kuhamia kwenye mtambo mwingine nilifanya tafiti na kuona watumiaji wengi wakilalamikia windows Vista hivyo niliamua kuachana nayo,habari njema ikaja na Microsoft wakaamua kuiondoa sokoni na kuleta Windows 7 ambayo ni kipenzi cha wengi. Hivyo TAFITI TAFITI TAFITI.
Hivyo kuwa makini kila unapokubali ujumbe wowote.Hakikisha unajua unachokifanya.
Hayo ni mabo machache ambayo unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira salama na yenye kinga bora.

Mazingatio.
- 1.Ondoa programu ambazo hauzitumii ili kupunguza uwezekano wa matatizo,wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kusimika programu nyingi wakati nyingi kati ya hizo huwa hatuzitumii kabisa,hizi programu hujaza nasafi,kuweka uchafu na hatimaye kutuweka hatiani.
- 2.Hakikisha unatumia programu zilizo kwenye wakati,simika maboresho(update) pindi yanapotokea.Nimeshuhudia watu wengi wamekuwa wagumu kusimika haya matoleo mapya kutokana na hofu mbalimbali.Achana na hofu.Maboresho yanakuja kwa ajili ya mambo mema na si kukudhuru.
II.Tumia programu za uhakika

Kwa kufanya hivi itakusaidia unapata programu ambayo inakidhi mahitaji yako huku ukiwa salama.Mfano mzuri binafsi sijawahi kutumia Windows Vista,kwani kipindi natumia Windows XP na kutaka kuhamia kwenye mtambo mwingine nilifanya tafiti na kuona watumiaji wengi wakilalamikia windows Vista hivyo niliamua kuachana nayo,habari njema ikaja na Microsoft wakaamua kuiondoa sokoni na kuleta Windows 7 ambayo ni kipenzi cha wengi. Hivyo TAFITI TAFITI TAFITI.
III.Hakikisha unajua nini unachokifanya
Wengi wetu tumekuwa wahanga kutokana na kukubali kiholela au kufanya mambo tusiyoyajua.Labda nikupe mfano mmoja wa mtu wangu wa karibu ambaye aliwahi kuvamiwa na na hizi programu za matangazo(Adware).Yeye alikuwa alifungua tovuti moja mara akaona ujumbe unasema kompyuta yako ipo hatarini hivyo bonyeza hapa ili kutatua.Bila kujua anachokifanya akabofya na kujikuta ameshaingiza madudu kibao.Hivyo kuwa makini kila unapokubali ujumbe wowote.Hakikisha unajua unachokifanya.
Hayo ni mabo machache ambayo unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira salama na yenye kinga bora.
No comments:
Post a Comment